Mobile Kilimo ni teknolojia ya simu ambayo itawasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupata masoko ya mazao yao bila ya kuangaika bali kwa njia ya simu zao za mkononi.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo teknolojia inakuja kwa kasi sana kwani takwimu zinaonesha watu karibu milioni ishirini na moja wanamiliki simu za mkononi.

Kwahiyo, karibu wakulima elfu tisini hawataangaika kutoa taarifa za mazao yao kwenye teknolojia hii. Wataweza kutoa taarifa za mazao, bei ya mazao na mahali walipo ili wanunuzi waweze kuwafikia kwa urahisi.

Mobile Kilimo kwa sasa inatoa maelezo hayo na maelezo ya jumla kuhusu kilimo kwa teknolojia ya simu- Asante kwa maendeleo ya kiteknolojia, wakulima, wafugaji, na wavuvi watafaidikika sana na huduma ya Mobile Kilimo.